Msanii nyota nchini Nadia Mukami ameachia EP yake mpya ambayo ni zawadi kwa mashabiki zake na shukran kwa mwenyezi Mungu baada ya kujifungua salama.
EP hiyo inakwenda kwa jina la Bundle of Joy ina jumla ya nyimbo 4 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Arrow boy, Latinoh na Iyanii.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Nadia Mukami amesema EP hiyo aliitengeneza kipindi yupo na ujauzito wa Mtoto wake wa Kiume haseeb kai huku akidai kwamba aliwekeza moyo wake wote kwenye Bundle of Joy EP.
EP hiyo ambayo ina nyimbo kama Zawadi, Kai wangu, Acheni Mungu aitwe Mungu, na Salute kwa Mama inapatikana kwenye digital platforms mbali mbali za kustream muziki duniani ikiwemo boomplay.
Bundle of Joy ni EP ya pili kwa mtu mzima Nadia Mukami ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2020 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo African Pop star iliyokuwa na jumla ya mikwaju 7 ya moto.