You are currently viewing Nadia Mukami afunguka juu ya mpango wa kupata mtoto wa pili

Nadia Mukami afunguka juu ya mpango wa kupata mtoto wa pili

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami amefichua kuwa hana mpango wa kupata mtoto mwingine hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram akimjibu shabiki aliyetaka kujua ni lini atampata mtoto wake wa pili, Nadia amesema kwa sasa hajajiandaa kisaikolojia kupata uja uzito mwingine huku akisisitiza kuwa atafanya hivyo labda miaka mitano ijayo.

“Labda baada ya miaka mitano, sitaki saa hii! Eh ni kujitolea pakubwa sana,” Mukami alisema.

Nadia kwa sasa ni mama ya mtoto mmoja aitwaye Kai aliyepata na mchumba wake Arrow Boy miezi minane iliyopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke