Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka tusiyoyajua kuhusu safari yake ya kumlea na kumnyonyesha mtoto wake wa kiume Hasib Kai ambaye ana umri wa miezi miwili.
Katika kikao cha maswali na mashabiki zake kwenye mtandao wa Instagram Nadia Mukami amesema ameongeza uzito kutoka kilo 55 hadi 63 jambo ambalo amedai limechangiwa na yeye kula chakula kingi ili aweze kumnyonyesha mtoto wake bila kizingiti.
Mbali na hayo hitmaker huyo wa ngoma ya “Zawadi” ameweka wazi baadhi ya vitu ambavyo alikuwa hapendi alipokuwa mjazito kwa kusema kwamba hakuwahi vutiwa na nyama ya ngombe, maziwa pamoja na mkate.
Hata hivyo kauli ya Nadia Mukami imezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wamempongeza kwa hatua ya kumpa mtoto wake kipau mbele kwenye malezi tofauti na wanawake wengi ambao hawapendi kuwanyonyesha watoto wao kwa ajili ya kulinda urembo wao.