Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amefunguka kuhusu madai ya kutengana na baba ya mtoto wake Arrow Bwoy.
Katika mahojiano na Mungai Eve, Nadia amesema kuwa alitengana na Arrow Bwoy baada ya kulemewa na mambo mengi ambayo yalitokea katika maisha yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
“Imekuwa moja ya miaka mbaya zaidi kwangu. Mungu amenibariki na pia nimepitia changamoto kwa viwango sawa. Nimepitia mengi, mambo yanaweza kuwa makubwa na inaweza kufikia mahali ukavunjika,” alisema.
Aidha amewasuta watu ambao walidai alikuwa akifanya kiki kwa ajili ya kutangaza biashara yake mpya ya urembo iliyofunguliwa jijini Nairobi mapema wiki hii.
“Haiwezi kuwa mbinu ya kutangaza biashara. Iliikuwa ni sadfa tu. Watu wanaoweza kunielewa wanajua kwamba nimeolewa hivi majuzi, nimepata mtoto na inaweza kulemea mtu, utapanga virago, ni mambo mengi,” alisema
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema licha ya kutengana na baba ya motto wake bado wanasaidia majukumu ya kuwalea motto wao, Haseeb Kai ikizingatiwa kuwa bado wanaisha katika nyumba moja.
Lakini pia amezungumzia ishu ya Eric Omondi kumkosoa kwa kushindwa kuwekeza kwenye suala la branding katika mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa amejifunza kitu kwenye kauli ya Omondi na atalifanyia kazi suala hilo.
Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya kuzindua biashara yake iitwayo ‘Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’ ambayo itahusika na masuala yote ya urembo.
Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’, nadia alisema uzinduzi wa biashara yake hiyo ni moja kati ya ndoto ambazo amekuwa akitamani kufanikisha katika maisha.