Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ameshindwa kuvumilia kinachoendelea mtandaoni kuhusu uja uzito wake na Arrow boy.
Kupitia video aliyoishare kwenye ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami amedokeza kuwa alipoteza uja uzito wake mwishoni mwa mwaka wa 2021.
Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” amesema licha ya kupoteza uja uzito wake aliahuma kutoweka wazi habari hiyo mbaya kwa umma.
Hata hivyo amemtolea uvivu Jalang’o kwa madai ya kusema kuwa hataomba msamaha kwa hatua ya kuanika uja uzito wake akiwa redioni akisema kwamba kitendo hicho sio cha kingwana..
Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya Jalang’o kutangaza redio kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mchumba wake Arrow Boy hivi karibuni.
Jambo ambalo lilimkasirisha Arrow Boy ambapo alitumia instastory kumuonya Jalang’o akome kuingilia maisha yake na nadia mukami.
Kutokana na hilo Jalang’o alimjibu Arrow Boy kwa kusema kwamba atakoma kuzungumzia maisha yao na hajutii kuweka wazi uja uzito wa Nadia Mukami.