You are currently viewing NADIA MUKAMI AFUNGUKA MENGI KUHUSU WAKFU WA LOLA & SAFARI, KUADILI DINI NA MSANII WAKE LATINOH

NADIA MUKAMI AFUNGUKA MENGI KUHUSU WAKFU WA LOLA & SAFARI, KUADILI DINI NA MSANII WAKE LATINOH

Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka sehemu ambayo wanapata ufadhili wa wakfu wao Lola na Safari ambao unalenga kuwasaidia wasichana wenye umri mdogo waliopata watoto wakiwa wajanga.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Nadia amesema wamekuwa wakipata usaidizi kutoka kwa makampuni wanayofanya kazi nao lakini pia kutoka kwa wahisani na marafiki zao huku akitoa wito kwa yeyote anayetaka kutoa msaada wowote kufanya hivyo bila kusita ili waweza kuwasaidia watu wenye uhitaji kwa jamii.

Hitmaker huyo wa “Zawadi” amesema wataendelea kurudisha fadhila kwa jamii bila kukoma huku akidokeza ujio wa tovuti ya wakfu wao wa lola na safari ambao waliuzindua kumuenzi mtoto wao aliyefariki mwaka jana kabla hajazaliwa.

Mbali na hayo, Nadia amefunguka kuhusu ishu ya kubadili dini kwa kusema bado hajapata shinikizo kutoka kwa mchumba wake arrow boy huku akisisitiza kuwa hana mpango wa kufanya hivyo kwa kuwa upendo ndio dini iliyowaleta pamoja.

Kuhusu msanii wake Latinoh, Nadia mukami amesema msanii huyo aliye chini lebo yake ya seven hub creative ataanza kuachia kazi zake mfululizo bila kupoa kama msanii huru hivi karibuni ikizingatiwa kuwa tayari wamefanya ngoma mbili pamoja ambazo Zawadi na Siwezi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke