Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ametolea uvivu Eric Omondi baada ya mchekeshaji huyo kudai wasanii wa kenya wataendelea kudharauliwa hadi pale watakapoacha tamaa na uzembe kwenye kazi zao za muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka Omondi aache suala la kujipendekeza katika ishu ya kupigania mabadiliko kwenye muziki wakenya ikizingatiwa kuwa ni suala mtambuka ambalo linahitaji kuzungumziwa kwa kina.
Hitmaker huyo “Roho Mbaya” ameenda mbali na kuonyosha maelezo kuhusu ya kufukuzwa na promota kwenye tamasha lilofanyika majuzi huko Mombasa kwa kusema kwamba hakutaka kupishana na waandaji wa tamasha hilo kwani hapendi kutumia nguvu kwenye kazi zake.
Kauli ya Nadia Mukami inakuja mara baada ya kudaiwa alitimuliwa na msanii mwenzake Masauti wakiwa jukwaani kumpisha msanii wa bongofleva mbosso kwenye tamasha la Bright Future lilofanyika mombasa wikiendi hii iliyopita.