Uongozi wa lebo ya Sevens Hub Creative umemtambulisha msanii wao mpya.
Lebo hiyo inayomilikiwa na msanii Nadia Mukami imemtambulisha msanii aitwaye latinoh mwenye umri wa miaka 21 kutoka Likoni, Mombasa kuwa msanii mpya chini ya lebo hiyo
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia Mukami amemtambulisha msanii huyo kwa kuandika ujumbe wa kumsifia akisema kuwa uwezo wake wa kuandika nyimbo, melody na vocals ndio baadhi ya vitu vilivyomshawishi kumsajili latinoh kwenye lebo ya Sevens Bub Creative.
Hitmaker huyo “Wangu” amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini lakini pia wakae mkao wa kula kupokea nyimbo zake.
Tayari Latinoh ameachia wimbo wake mpya uitao Siwezi ambao amemshirikisha Nadia Mukami na unapatikana kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.
Lebo ya Sevens Creative Hub ni kati ya lebo kubwa nchini Kenya ambazo zinafanya vizuri kwa sasa.