You are currently viewing NADIA MUKAMI ANYOSHA MAELEZO KUHUSU TETESI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKE ARROW BOY

NADIA MUKAMI ANYOSHA MAELEZO KUHUSU TETESI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKE ARROW BOY

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amekanusha madai ya kumu unfollow mchumba wake Arrow Boy kwenye mtandao wa Instagram.

Akijibu shabiki yake kwenye mtandao wa instagram aliyetaka kujua hali ya uhusiano wake kwa sasa na Arrow Boy, Nadia Mukami amesema hajawahi fuatilia na Arrow Boy kwenye mtandao huo huku akithibitisha kuwa uhusiano wake na hitmaker huyo wa ngoma ya Unconditional Love upo imara licha ya uvumi unaosambaa mitandaoni kuwa hawana maelewano mazuri.

Nadia Mukami ameyaweka hayo wazi wakati akitangaza ujio wa album mpya  ya Arrow boy iitwayo Focus inayotarajiwa kuingia sokoni machi 12 mwaka wa 2022.

Mapema wiki hii mitandao nyingi ya udaku nchini iliripoti kuwa uhusiano wa Nadia Mukami na Arrow Boy umeingia na ukungu mara baada ya wasanii hao kutoonekana wakifuatilia kwenye mtandao wa Instagram.

Utakumbuka Mwezi agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu.

Hitmaker huyo wa Maombi alienda mbali na kueleza kuwa aliahamua kuyaweka wazi mahusiano yake na Arrow Boy kwa sababu tayari alikuwa amekuwa kiakili kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke