You are currently viewing Nadia Mukami atangaza kuingia gym kupunguza mwili wake

Nadia Mukami atangaza kuingia gym kupunguza mwili wake

Baada ya kusemwa sana mitandaoni kuwa amenenepa kupita kiasi na kupoteza mvuto tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza na Arrow Boy, msanii Nadia Mukami ameamua kuingia gym kwa ajili ya kupunguza mwili wake.

Nadia Mukami amechukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wasanii wenzake pamoja na mashabiki wake kutopendezwa na unene wake kwani unamfanya kuonekana kituko kwenye jamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia amekiri kuteswa na unene kiasi cha kuingiwa na uoga wa kuchapisha picha au video zake kwenye mitandao ya kijamii huku akiapa kufanya mazoezi makali ambayo yatamsaidia kukata uzito wa mwili wake kutoka kilo 67 hadi 60.

Hata hivyo, baada ya kuanza mazoezi magumu , watu wengi wamempongeza Nadia Mukami kwa hatua hiyo huku baadhi ya mashabiki wakisema wanasubiri kumuona msanii huyo akirejesha muonekano wake wa awali lakini asijikondeshe kupita kiasi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke