Hitmaker wa Maombi, msanii Nadia Mukami ametangaza kuwa ana jambo lake kubwa la kufungia mwaka.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema mwezi Desemba mwaka huu ana shughuli ambayo atazindua kwa ajili ya mashabiki zake.
“Launching Something this December,” Aliandika insta-story
Hata hivyo haijajulikana ni nini hasa msanii huyo atazindua ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda ni mipango ya kuachia Album yake mpya ambayo juzi kati alitusanua kuwa itaingia sokoni mapema mwaka 2023.