You are currently viewing NADIA MUKAMI AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA ARROW BOY

NADIA MUKAMI AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA ARROW BOY

Msanii nyota nchini Arrow Boy amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Nadia Mukami ambaye pia ni mwanamuziki.

Kwenye performance yao  katika hafla ya uzinduzi wa Focus album Usiku wa kuamkia Machi 13 jijini Nairobi, Arrow Boy alipiga goti na kumvisha Pete Nadia Mukami ambapo alienda mbali zaidi na kuahidi yupo tayari kufunga nae ndoa,  jambo lilomfanya Nadia Mukami amwage machozi ya furaha huku mashabiki wakiwashangilia kwa hatua ya kuanika wazi mahusiano yao.

Haya yanajiri ikiwa ni  siku chache baada ya Wawili hao kuweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kwenye uzinduzi wa wakfu wao wa “Lola & Safari”

Utakumbuka Mwezi Agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami pamoja na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke