You are currently viewing NADIA MUKAMI AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI

NADIA MUKAMI AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amewajibu wanaomkosoa kwenye mitandao wa kijamii kutokana na mavazi aliyovalia juzi kati kwenye onesho lake huko Meru.

Nadia kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram amesema licha ya watu kukosoa mavazi yake mtandaoni onesho lake huko Meru ilipata mapokezi mazuri, ambapo ameenda mbali na kudai kuwa yeye ni moja kati wanawake ambao huwa hawakati tamaa kirahisi kwa sababu ni mpambanaji.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Zawadi amesema ataendelea kutia bidii kuhakikisha muziki wake unawafikia wengi kwani anafahamu kwamba wasanii wengi wa kike wamekuwa wakipitia changamoto nyingi kukubalika kwenye tasnia ya muziki nchini haswa baada ya kuwapata watoto katika maisha yao.

“Now that I got your attention with the outfit, the event was successful. I am not a woman who gives up, I work hard. It is even harder when you have given birth, and you are a female artist. I alone, understand what I have been going through. It is challenging I have addressed the issues female artistes go through after giving birth.” Ameandika Instagram.

Utakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa Nadia Mukami kushambuliwa mtandaoni, mwaka wa 2020 watu walimtupia kila aina ya matusi kiasi cha kutangaza kuchukua mapumziko mafupi kwenye mitandao ya kijamii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke