Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ametangaza rasmi ujio wa album yake mpya na ya kwanza katika muziki wake.
Kupitia ukurasa wake wa instagram amesema yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kukamilisha album yake mpya ambayo itaingia sokoni mapema mwaka 2023.
“I am working on my Album! The best thing I can do is starve my fans just a little bit! Early Next year, y’all getting an Album!Sending Love to my Fans! kaNadians!”. Aliandika
Mara ya mwisho Nadia Mukami kuwabariki mashabiki na kazi ilikuwa miezi sita iliyopitia alipoachia Bundle of Joy EP yenye jumla ya mikwaju 4 ya moto.