Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha wimbo wake wa Tesa aliyomshirikisha fena Gitu na Khalighraph Jones kuondolewa kwenye mtandao wa youtube kwa madai ya hakimiliki.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami amehapa kupambana na msanii aliyesababisha wimbo wake kuondolewa kwenye mtandao wa youtube kwa kusema kwamba yupo tayari kutumia pesa zote alizochuma kupitia muziki wake kuhakikisha kwamba aliyesusha wimbo wake youtube anachukulia hatua kali za kisheria.
Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” ametoa ya moyoni na kuwataka wanaoendeleza kadhia hiyo kukoma mara moja kwani wamewapelekea wasaniii wengi kupata hasara ikizingatiwa kuwa wasanii hutumia pesa nyingi kuandaa video za nyimbo zao.
Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya msanii chipukizi kudai kwamba mrembo huyo aliiba idea yake na kuitumia kwenye wimbo wa Tesa bila ya kumshirikisha.