You are currently viewing NADIA MUKAMI KUMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA HIVI KARIBUNI

NADIA MUKAMI KUMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA HIVI KARIBUNI

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametangaza kumtambulisha msanii wake mpya chini lebo ya muziki ya Sevens Creative hub mwanzoni mwa mwaka wa 2022.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema atamsaini msanii wake mpya chini ya Seven Creative Hub mwezi Januari mwaka wa 2022 ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kumpokea msanii huyo ambaye pia ataachia video ya wimbo wake mpya ambayo amemshirikisha baada ya utambulisho wake.

This January I am introducing my New artist and our First video together Drops!!! Are you ready???? @sevenscreative_hub..ameandika Nadia Mukami kupitia Instagram page yake.

Hata hivyo hajaweka wazi jinsia ya msanii huyo ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda msanii huyo akawa Slyvia Ssaru ambaye kipindi cha nyuma alinukuliwa kwenye instagram yake akisema mwakani atasainiwa na lebo ya Sevens Creative hub ambayo inamilikiwa na Nadia Mukami.

Haikushia mbali zaidi na kuwataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea ujio mpya kwani ataachia rasmi Extended Playlist yake baada ya kuingia ubia wa kufanya kazi na Sevens Creative hub.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke