You are currently viewing NADIA MUKAMI KURUDISHA FADHILA KWA JAMII KUPITIA LOLA & SAFARI FOUNDATION

NADIA MUKAMI KURUDISHA FADHILA KWA JAMII KUPITIA LOLA & SAFARI FOUNDATION

Msanii Nadia Mukami amehamua kurudisha fadhila kwa jamii kupitia wakfu wake wa Lola & Safari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia Mukami amesema siku ya kina Mama Duniani Mei 8, wakfu wa Lola & Safari umeamua kuandaa hafla ya kuwasherekea kina mama wenye umri mdogo huko jijini Nairobi ambapo watatoa elimu na msaada wa vyakula na mavazi kwao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Maombi” amesema hakuna mtoto wa kike anapaswa kukatisha ndoto zake kutokana na mimba za mapema kwani kupitia Lola & Safari watafunzwa jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.

Utakumbuka Lola & Safari ni wakfu ambao ulizinduliwa kabla ya Nadia Mukami hajajifungua mtoto wake Hasib Kai na ililenga kusaidia kina mama wenye umri mdogo ambao wametelekezwa na watu wao wa karibu.

Wakfu wa “Lola and Safari Foundation” iliyo chini ya Nadia Mukami na Arrow Bwoy tayari imewapatia dili la Ubalozi wa hospitali ya Ruai Family Hospital (RFH)

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke