You are currently viewing NADIA MUKAMI: MIMI SIO MTU WA KIKI, KIKI ZINANIFUATA ZENYEWE

NADIA MUKAMI: MIMI SIO MTU WA KIKI, KIKI ZINANIFUATA ZENYEWE

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amefunguka na kudai kuwa yeye siyo mtu wa kupenda kiki kama baadhi ya watu wanavyodai kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Nadia Mukami amesema yeye haitaji kiki ili kazi zake ziweze kufanya vizuri, tofauti na wasanii wengi wa kizazi kipya.

Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” amedai vitu vingi anavifanya katika hali ya kawaida lakini vinakuzwa na media hali ambayo amedai kwake haoni kama ni tatizo kwani ataendelea kutoa muziki mzuri bila kujihusisha na kiki.

Nadia Mukami amekuwa akitawala mitandao ya kijamii kila kukicha kutokana na vituko vyake huku watu wakidhani huenda akawa anapanga kufanya matukio ya namna hiyo ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke