You are currently viewing NADIA MUKAMI NA MEJJA MBIONI KUACHIA COLLABO MATATA

NADIA MUKAMI NA MEJJA MBIONI KUACHIA COLLABO MATATA

Staa wa muziki nchini Nadia mukami ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirisha mkali wa muziki nchini Mejja

Kupitia ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami Amepost clip fupi kutoka kwenye wimbo wake mpya na mejja huku akiwataarifu mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea ngoma yao mpya kwa jina la “Legeza” ambayo itaachiwa rasmi Novemba 9 mwaka huu ambapo itapatikana kwenye digital platforms mbalimbali za muziki.

Hii itakuwa kazi ya kwanza kwa Nadia mukami na Mejja ikiziingatiwa kuwa wawili hao hawajai fanya wimbo wa pamoja.

Mara ya mwisho Nadia Mukami kuachia kazi ilikuwa ni mwezi Julai mwaka huu ambapo aliachia wimbo uitwao “Roho Mbaya” na mpaka sasa video ya wimbo huo inaendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube kwani imefanikiwa kufikisha zaidi ya watazamaji millioni 1.2.

Ikumbukwe Nadia Mukami kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya album yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka wa 2021

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke