Kundi la muziki kutoka Tanzania, Navy Kenzo limeonyesha kupuuzia madai kuwa wamepotea tangu kuachia kolabo yao na Diamond Platnumz, kupitia wimbo uitwao “Katika”.
Memba wa kundi hilo, msanii Nahreel amepangua kauli hiyo kutoka kwa shabiki mmoja ambaye aliacha komenti kwenye ukurasa wa instagram wa Nahreel, kwa kuandika; “Diamond mbaya sana toka mfanye naye wimbo dah, hamsikiki naumia sana”, Nahreel alimjibu shabiki huyo kwa kumuandikia; “Kaa mkao wa kula”.
“Katika” ni kolabo iliyowakutanisha Navy Kenzo na Diamond Platnumz, ilitoka mwaka 2018.
Ikumbukwe Navy Kenzo kwa sasa wanajiandaa kuachia album yao ya nne baada ya kuachia Hold Me Back ya mwaka 2015, AIM – Above Inna Minute ya mwaka wa 2017 na Story Of The African Mob ya mwaka 2020.