You are currently viewing NAHREEL WA NAVY KENZO AKANUSHA MADAI YA KUPOKONYWA NYOTA YAO NA DIAMOND PLATNUMZ

NAHREEL WA NAVY KENZO AKANUSHA MADAI YA KUPOKONYWA NYOTA YAO NA DIAMOND PLATNUMZ

Msanii na Prodyuza, Nahreel kutoka kundi la Navy Kenzo amesema sio kweli kwamba Diamond Platnumz anachukua nyota za wasanii mwenzake kupitia kolabo bali ni mipango ya wasanii wenyewe.

Akizungumza hilo, Nahreel amesema mashabiki huwa wanaongea vitu vingi na ni haki yao kwa sababu wanahitaji huduma yao mara kwa mara, wanapokaa kimya wanaona kama wamepotea au kuchukuliwa nyota lakini sio kweli.

“Hayo mambo ya kuchukuliana nyota sio kweli, sisi tunapitia changamoto nyingi, hata ambao wanawaona sehemu nzuri juu hata wenyewe pengine kuna changamoto wanapitia” amesema Nahreel.

Nahreel amesema wanapenda kufanya kazi kwa mipango kwa sababu wanaweka nguvu nyingi kwenye ubunifu na namna ya kuandaa muziki na video, hivyo wanatakiwa kuwa watulivu katika kuandaa kitu kizuri.

“Mambo ya nyota hapana, tumekaa kimya kwa sababu ya vitu vingi, sio muziki tu, tuna Academy ya mpira, Aika ana biashara zake, kwa hiyo tumekuwa tukiweka nguvu huku ili mambo yaende, baadaye muda mzuri ukifika tunaweka tena nguvu kwenye muziki,” amesema.

Hata hivyo amesema wao kama Navy Kenzo wamekuwa wakifanya muziki kwa muda mrefu, hivyo ni vigumu kusema watakuwa wanafanya tu muziki, lazima wewe wanajihusisha na vitu vingine.

Utakumbuka Septemba 28, mwaka wa 2018 Navy Kenzo waliachia video ya wimbo wao, Katika waliomshirikisha Diamond, hadi sasa video yake katika mtandao wa YouTube imepata views milioni 26.1 na kuwa video yao pekee iliyotazamwa zaidi.

Lakini tangu wakati huo hakuna video yoyote waliyotoa Navy Kenzo iliyofanikiwa kufikisha walau views milioni 1 licha ya kuachia ngoma kali kama Roll It, Magical, Why Now, Bampa 2 Bampa, Only One na Nisogelee.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke