Mkali wa muziki nchini Naiboi amefunguka sababu za kukaa kimya kwenye muziki wake kwa takriban miaka miwill.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Naiboi amesema kwa muda sasa mashabiki zake wamekuwa wamkishinikiza atoe nyimbo mpya ila uongozi wake umekuwa kizingiti kwake kufanya hivyo.
Hitmaker huyo wa pesa amesema ameumizwa na kitendo cha kukaa kimya kwenye muziki wake ikizingatiwa kuwa amerekodi zaidi ya nyimbo 800 za moto ambapo amewataka mashabiki zake waendelea kumuombea arejee katika hali yake ya kawaida.
Ikumbukwe Naiboi amekuwa akitangaza ujio wa Ep yake iitwayo Otero ambayo hajeweka wazi itaingia lini sokoni.
|