You are currently viewing NAIBOI ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA OTERO EP

NAIBOI ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA OTERO EP

Mkali wa muziki nchini Naiboi ametoa taarifa muhimu kwa mashabiki zake kuhusiana na ujio wa EP yake iitwayo Otero EP.

Akipiga stori na pulse Naiboi amethibitisha EP yake mpya Otero itatoka rasmi Oktoba mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto.

Awali EP hiyo ilikuwa itoke Oktoba 8 mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wa Naiboi.

Taarifa ya ujio wa Otero EP inakuja wiki kadhaa baada ya naiboi kufunguka kuhusu ukimya wake kwenye muziki akisema kuwa uongozi wake ulikuwa kizingiti kwake kuachia project mpya ikizingatiwa kuwa ana zaidi nyimbo 800 ambazo amesharekodi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke