You are currently viewing NAMELESS AWAONYA VIJANA DHIDI YAKUTUMIWA NA WANASIASA TAIFA LINAPOJIANDAA KWA UCHAGUZI MKUU

NAMELESS AWAONYA VIJANA DHIDI YAKUTUMIWA NA WANASIASA TAIFA LINAPOJIANDAA KWA UCHAGUZI MKUU

Lejendari wa muziki nchini Nameless amewaonya vijana dhidi ya kutumiwa na baadhi ya wanasiasa ili kuwakuza kisiasa.

Katika mahojiano na Mpasho Nameless amesema ahadi zinazotolewa na baadhi ya mirengo ya kisiasa ni njama ya kuwahadaa vijana ili kuwaunga mkono katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Back It Up” amewataka vijana kujiepusha na siasa za chuki na ukabila na badala yake kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani kote nchini.

Nameless amesema hayo kwenye uzinduzi wa mpango wake wa Pride ya Kenya ambao unalenga kuwahimiza vijana kutokubali mawazo hasi kuathiri ndoto zao katika maisha kupitia sanaa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke