You are currently viewing NAMELESS NA WAHU WANATARAJIA MTOTO WA TATU

NAMELESS NA WAHU WANATARAJIA MTOTO WA TATU

Wanamuziki David Mathenge maarufu kama Nameless na Wahu Kagwi wametangaza kwamba wanatarajia mtoto wao wa tatu.

Wawili hao walitoa tangazo hilo kupitia video ambayo waliichapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Tumiso ndiye kifungua mimba wa wanamuziki hao ambao walifunga ndoa mwaka 2005 na wa pili ni Nyakio.

Ndoa ya wanamuziki hao imedumu muda mrefu kinyume na matarajio ya wengi kutokana na jinsi watu maarufu wamekuwa wakiacha ndoa zao ulimwenguni kote.

Utakumbuka kwa sasa Wahu na Nameless wanafanya vizuri na wimbo wao mpya uitwao Deep, wimbo ambao ni wa sita kutoka kwenye album yao ijayo iitwayo MZ.

Tayari wameachia nyimbo kama This Love Ya Wahu, This Love Ya Nameless, Te Amo, Feeling na Back it Up.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke