Staa wa muziki wa bongofleva Nandy ameanika mkeka wake kwa mwaka 2022 upande wa Kolabo na wasanii wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa instagram hitmaker huyo wa “Yuda” ametangaza Kolabo yake na Davido pamoja na Patoranking wa Nigeria.
Mbali na hao, ametangaza pia kuwa na ngoma nyingine na Sauti Sol baada ya “Kiza Kinene” iliyotoka miaka miwili iliyopita.
Kolabo nyingine aliyotupasha Nandy ni ile alitusanua mwaka jana aliyosema atafanya na msanii wa singeli nchini tanzania Dulla Makabila.
Hata hivyo ameachia mashabiki zake swali, aanze na collabo kati ya hizi ambazo ameziweka wazi huku pia Akisema kuwa mikakati ya kuja na tamasha lake la nandy festival 2022, hivyo Mashakibi wakae mkao wa kula mambo mazuri yanakuja kutoka kwake.