Staa wa muziki wa Bongofleva Nandy amethibitisha rasmi kuwepo na shida kwenye akaunti yake rasmi ya mtandao wa Instagram ambayo ina followers milioni 6.3
Kwa mujibu wa nyanzo vya habari za burudani kutoka nchini Tanzania, akaunti ya msanii huyo imekuwa disabled (imefungwa) na Instagram wenyewe baada ya jaribio la kudukuliwa na mtu ambaye bado hajafahamika.
Hata hivyo duru za kuaminika zinasema uongozi wake upo kwenye hatua za kuirejesha akaunti hiyo.
Utakumbuka kando na kujitangaza, miaka ya hivi karibuni akaunti za mastaa wa muziki zimekuwa moja ya vyanzo vyao muhimu vya kipato na wale wenye followers wengi wamekuwa wakipata deals zenye hela nyingi.