Mwanamuziki wa Bongofleva Nandy kwa mara ya kwanza ameweza kufunguka machache kuhusiana na ujauzito wake.
Akizungumza kwenye sherehe ya ‘kitchen party’ yake wikiendi hii iliyopita Nandy amesema, mumewe mtarajiwa (Billnass) ndio wa kwanza kugundua kuwa ana ujauzito mara baada ya kuona mabadiliko mbalimbali kama ya kitabia.
Lakini pia amebainisha kitu alichokuwa akikitamani ni kupata mtoto akiwa tayari yupo ndani ya ndoa, hivyo kwa namna ilivyotokea amesema ni baraka pia.
“Nilikuwa natamani kupata mtoto nikiwa tayari nipo ndani ya ndoa. Nimejaliwa nikiwa bado sijaingia kwenye ndoa lakini huyu mtoto ntaingia nae kwenye harusi na kwenye ndoa hivyo sio kitu kibaya ni baraka na wazazi wote wameridhia” – ameeleza Nandy.
Ikumbukwe, Nandy na Billnass ambao kwa sasa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni, wana mpango kufungua ndoa mwezi huu wa Julai.