You are currently viewing NANDY AFUNGUKA KUJISIKIA VIBAYA RAYVANNY KUTOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 2

NANDY AFUNGUKA KUJISIKIA VIBAYA RAYVANNY KUTOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 2

Staa wa muziki kutoka Tanzania Nandy kwa mara ya kwanza amefunguka jinsi alivyojiskia baada ya kusikia msanii Rayvanny anatakiwa alipe kiasi cha pesa cha shilingi milioni 2 kama faini ya kutokufuata mikataba na lebo yake ya WCB.

Kupitia mahojiano yake na Clouds Media Nandy amedai kuwa alifanya mawasiliano na msanii moja kwa moja na sio record label ya WCB baada ya taarifa za mwanamuziki huyo kujiengua kwenye record label hiyo, na alijiskia vibaya baada ya kusikia stori hizo japo kuwa hana uhakika nazo maana zimezuka tu mitandaoni.

“Nimeziona hizo taarifa na nimejisikia vibaya maana nimeona kama mimi ndio niliosababisha hivyo lakini niliona katika instastory yake kuwa ameandika yeye ni msanii huru hivyo sikuamini kama kalipishwa maana si unajua tena stori za mitandaoni” Alisema Nandy.

Utakumbuka baada ya Rayvanny kutokea kama surprise kwenye tamasha la Nandy Festival 2022 huko Songea nchini Tanzania na kuzuka stori mitandaoni kuwa lebo yake ya zamani ya WCB imemuhitaji kulipa kiasi cha pesa cha milioni 2kwa kosa la kukiuka mikataba walioingia kwa kwenda kutumbuiza katika tamasha hilo.

Mbali na hayo amesema kwa sasa miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni pamoja na marafiki wa mume wake Billnass

“Sipendi marafiki wa mume wangu na wanalijua hilo wananiambiaga mimba hiyo inakusumbua kuna muda napokea simu zake nawaambia muacheni analea mimba”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke