Msanii wa muziki wa bongofleva Nandy ametoa pole kwa watu wote waliotapeliwa kwa jina lake kwenye mitandao ya kijamii.
Nandy ametoa pole hiyo katika taarifa yake ya wazi kuwa ahusiki na wanaotangaza kuwa ana SuperMarket inayoendesha utaratibu wa kutoa ajira kwa watu wakitumia kivuli cha jina lake.
Nandy ameeleza hilo kupitia Insta Story kwenye mtandao wa instagram akiongeza kuwa mbali na kuwa anaelewa changamoto ya ajira nchini tanzania lakini watu wawe makini wasitapeliwe na kwa upande wake hana mpango wa kufungua biashara ya namna hiyo.