Msanii wa Bongofleva, Nandy na mume wake, Billnass wamejaliwa kupata mtoto wao wa kwanza.
Akithibitisha taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Dr Cheni ambaye alikuwa MC wa harusi yao, amewapongeza wawili hao na kuwatakia afya njema pamoja na mtoto wao.
“Wow Congratulations Mr and Mrs Billnass na Nandy kwa kupata mtoto Mungu awakizie awalindie kitoto Chenu. Mbarikiwe sanaa” ameandika Dr Cheni.
Utakumbuka hivi karibuni Nandy alitangaza kusimamisha tamasha lake, Nandy Festival baada ya kupita kwenye mikoa miwili kati ya mitano nchini Tanzania iliyokuwepo kwenye ratiba yake