Msanii kike nchini Nasha Travis ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la The African Sound Queen Ep .
The African Sound Queen Ep ina jumla ya ngoma 6 za moto na bonus track moja ambazo zimetayarishwa na maprodyuza kama Kashkeed, Alexis on the beat, Bonga pamoja na Mumo beats.
Lakini pia mrembo huyo amewashirikisha wakali kama Madini Classic, Joefes, Japesa, Bonga de Alpha na DJ Lyta.
The African Sound Queen Ep ni Kazi ya kwanza kwa mtu mzima Nasha Travis tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.