Msanii wa kike nchini Nasha Travis amewaomba wasanii wa Kenya kupunguza kiki na kuongeza bidii katika muziki.
Katika mahojiano na podcast ya Nicholas Kioko kwenye mtandao wa Youtube, Nasha Travis amewataka wasanii nchini wazingatie suala la kutayarisha muziki mzuri badala ya kiki ambazo hazina msingi wowote.
Kulingana na Nasha, muziki ni kama bidhaa na mashabiki hutumia bidhaa hiyo kulingana na ubora wake.
Mrembo huyo kutoka Bar Nelson Empire amesema anatamani sana kuona wasanii wa Kenya wanajihusisha na muziki pekee na wala si masuala mengine ya kuwapa umaarufu mtandaoni.
Ikumbukwe kwa sasa Nasha Travis anafanya vizuri na EP yake mpya African Sound Queen ambayo iliingia sokoni Aprili mosi mwaka huu ikiwa na mikwaju 7 za moto.