Msanii Nasha Travis amedai kuwa kiki zinaweza kuwa na mchango fulani katika muziki wa msanii tofauti na watu wengi ambao hupinga suala hilo.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Nasha amesema anaona ni sawa tu kwa wasanii kutengeneza matukio ili wazungumziwe mtandaoni kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wao.
Katika hatua nyingine Mrembo huyo ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Naiwe” amesisitiza kuwa ingawa kiki ina mchango kwenye muziki, inapaswa kufanywa kwa ustaarabu kwani inaweza kuwa shubiri pale wasanii wanapotupiana maneno machafu mtandaoni.