You are currently viewing Navy Kenzo watajwa kushirikishwa kwenye album ya Kampuni ya EMPIRE

Navy Kenzo watajwa kushirikishwa kwenye album ya Kampuni ya EMPIRE

Kundi la muziki maarufu kutoka nchini Tanzania Navy Kenzo wametajwa kuwa ni moja wapo ya wasanii watakao unda tracklist ya album iliyoandaliwa na Kampuni ya usambazaji wa muziki ya EMPIRE iliyopo San Francisco, Marekani.

Taarifa hiyo ambayo imethibitishwa na ukurasa rasmi wa instagram wa Empire Africa pia ikiandikwa kwenye tovuti kubwa kama Billboard, Hot97 na Variety za nchini marekani, album hiyo inatajwa kuwa na mjumuisho wa mastaa wa muziki kutoka Afrika wakiwemo Olamide, Fireboy DML, Kizz Daniel, Buju BNXN, Asake, Black Sherif na wengineo wengi.

Album hiyo imepewa jina la “Where we come from” na inatarajiwa kutoka mwezi ujao, Novemba 18, 2022.

Utakumbuka Empire Africa wameamua kuja na album hii baada ya muziki kutoka barani Afrika kusikilizwa na kupendwa kwa kiwango kikubwa Duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke