Msanii wa Hiphop kutoka Tanzania Nay wa Mitego ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Atakuoa Nani” amewabarki mashabiki zake na “Rais Wa Kitaa Album” ambayo ina jumla ya nyimbo 14 za moto, ikiwa na kutoka kwa wakali kama Alikiba, Marioo, Jux, Mejjah, Maua Sama, AY, Shammy, Runtown na Kelechi Africana.
Album hiyo ambayo ni ya kwanza kwa mtu mzima Nay wa Mitego tangu aanze safari yake ya muziki kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki mtandaoni.
Utakumbuka mapema wiki hii iliyopita Nay wa Mitego alitajwa kuwania tuzo ya AFRIMA 2022 huko Nigeria kupitia vipengele viwili, Best Artist Of The Year na Song Of The Year.