You are currently viewing NAY WA MITEGO AMTOLEA UVIVU KUSAH, ADAI MAHUSIANO YAKE YANA PROMO KUBWA KULIKO MUZIKI

NAY WA MITEGO AMTOLEA UVIVU KUSAH, ADAI MAHUSIANO YAKE YANA PROMO KUBWA KULIKO MUZIKI

Rapa kutoka nchini Tanzania Ney wa Mitego  ameeleza kuwa msanii kusah ni msanii mzuri sana ,lakini watu wanashindwaa kumzingatia kwa sababu ya mambo yake ya mahusiano.

Ney wa Mitego amefunguka hayo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, akieleza kuwa hata yeye humsikiliza sana msanii huyo, lakini watu wanashindwa kumzingatia kwa sababu anaonekana mtu wa kulelewa kwenye mahusiano.

Hitmaker huyo wa “Rais wa Kitaa” amesema kusah hayupo serious na muziki wake kwani ameyapa mahusiano yake promo kubwa kuliko nyimbo zake.

Hata hivyo rapa huyo amemaliza kwa kumshauri msanii huyo kuchagua moja kati ya mahusiano ama muziki wake kwa kuwa bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke