Rapper kutoka nchini Tanzania Nay wa Mitego chini ya Uongozi wake wa Free Nation ametangaza rasmi kujitoa katika tuzo za muziki za Tanzania Music Awards.
Kupitia taarifa ya wazi aliyowekwa mtandaoni, ameeleza sababu za kufikia maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kutokua na imani na kamati ya uchambuzi wa kazi yaani (academy) ambapo amewataka mashabiki zake kusitisha mchakato wa kumpigia kura kwenye kipengele cha msanii bora wa rap aliyochokuwa akiwania na na Professor Jay ,Rapcha, & Young Lunya .
Aidha, tuzo hizo za muziki nchini Tanzania zinazoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) zinatarajiwa kutolewa Aprili mosi, mwaka wa 2022, huku vigezo vikubwa vilivyotumika kuwapata wasanii vikiwa ni wale waliopeleka kazi zao.