You are currently viewing NAZIZI HIRJI AOMBOLEZA KIFO CHA PRODYUZA MWAX THE HERBALIST

NAZIZI HIRJI AOMBOLEZA KIFO CHA PRODYUZA MWAX THE HERBALIST

Taarifa za kìfo cha prodyuza mkongwe nchini Mwax the Herbarlist imemuacha msanii wa muziki Nazizi Hirji na majonzi mengi kutokana na mchango wake kwenye tasnia ya muziki nchini.

Akizungumza na mpasho Nazizi ambaye alikuwa rafiki wa mwenda zake amemkumbuka prodyuza huyo kama moja ya watu waliokuwa nguzo muhimu kwenye muziki wake huku akisema kifo chake ni pigo kubwa kwa muziki wa Kenya.

Nazizi amesema Mwax amekuwa akiumwa tangu utotoni na walidhani kwamba ugonjwa uliokuwa ukimsumbua ungethibitiwa na madaktari lakini kwa bahati mbaya ametangulia mbele za haki kabla hilo halijafanikiwa.

Hitmaker huyo wa “Ni Sawa Tu” amewataka mashabiki kuendelea kumuombea mke pamoja na watoto wa prodyuza huyo wakati huu mgumu huku akisema kwamba huenda kifo cha mama yake mzazi ilimuathiri kisaikolojia.

Hata hivyo amedokeza Mwax The Herbalist atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Malindi, Kaunti ya Kilifi ikizingatiwa tayari kuna group la whatsapp ambalo limebuniwa kwa ajili kusaidia familia kufanikisha mazishi ya prodyuza huyo.

Mwax ambaye alikuwa mdogo wa msanii K-rupt aliyepoteza maisha yake mwaka wa 2003, alifariki Septemba 5 mwaka huu baada ya kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke