You are currently viewing NBA YOUNGBOY AACHIWA HURU KWA DHAMANA

NBA YOUNGBOY AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Baada ya takribani miezi saba kusota rumande, hatimaye rapper NBA YoungBoy ametoka jela kwa dhamana ya shillingi millioni 55.6 baada ya jaji wa Louisiana kumpa dhamana.

Rapper huyo ameripotiwa kuachiliwa huru kabla ya kifungo kuisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na tabia nzuri aliyoionesha.

Hata hivyo kwa sasa yupo kwenye kifungo cha nyumbani na atahitajika kuvaa kifundo cha mguu, lakini pia hawezi kuondoka katika makazi anayoishi na ni familia yake pekee inayoweza kuishi naye.

Rapper huyo ambaye alikamatwa mwezi Machi mwaka huu baada ya kufanyika kwa msako wa polisi na kukutwa na hatia ya kumiliki bunduki na bunduki hiyo kutokuwa na usajili, pamoja na kukutwa na dawa za kulevya.

Vikwazo vingine alivyowekewa ni pamoja na kutokuwa na silaha na kutojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambapo pia atatakiwa kuwa anawasiliana na watu wa idara ya kupambana na dawa za kulevya kwa vipimo vya mara kwa mara.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke