Mtayarishaji muziki kutoka Marekani DJ Mustard na mkewe Chanel Thierry wameripotiwa kuachana na shauri la talaka tayari limefika mahakamani.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Shauri hilo lilifunguliwa mnamo Jumatatu wiki hii.
Wawili hao walifunga ndoa Oktoba mwaka 2020 baada ya kuwa penzini tangu wakiwa na umri wa miaka 19.
Sababu ya kuachana kwao ni kushindwa kuelewana. Pamoja wamebarikiwa kupata watoto watatu; Kiylan wa miaka 10, Kauner wa miaka 7 pamoja na Kody wa miaka 2.