You are currently viewing NDOA YA KRG THE DON NA MKEWE LINAH WANJIRU LAFIKIA KIKOMO

NDOA YA KRG THE DON NA MKEWE LINAH WANJIRU LAFIKIA KIKOMO

Ndoa ya Krg The Don na mke wake Linah Wanjiru imevunjika rasmi baada ya miaka 8.

Hii ni kufuatia mahakama kutangaza rasmi kwamba Krg anaweza kuendelea na maisha yake ya U-single.

Pia mahakama hiyo imeliondoa jina la Krg kwenye majina matatu ya Linah Wanjiru  baada ya mchakato wa talaka kukamilika wiki hii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Krg ameshabiki hatua hiyo ya mahakama akisema kwamba watashirikiana kutoa matunzo kwa watoto wao huku akimtakia kila la heri aliyekuwa mke wake Linah Wanjiru kwenye maisha yake mapya.

Ikumbukwe, wawili hao wamedumu kwenye ndoa kwa takribani miaka 8 na wamebarikiwa kupata watoto wawili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke