You are currently viewing NDOA YA SIZE 8 NA DJ MO YAVUNJIKA

NDOA YA SIZE 8 NA DJ MO YAVUNJIKA

Mitandao mbali mbali ya burudani nchini imeripoti kuwa Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Size 8 Reborn ameikimbia ndoa yake mara baada ya kuingia kwenye ugomvi mkali na mume wake DJ Mo.

Vyanzo vya karibu na wawili hao vimesema Size 8 aliondoka nyumbani kwake wiki iliyopita pamoja na watoto wake wawili kutokana na vitendo vya usaliti.

Hata hivyo juhudi za marafiki na wanafamilia kuwalewata pamoja wawili hao hazikuzaa matunda kufutia hatua ya Size 8 kuwataka wampe muda wa kufikiria kuhusu hatma ya ndoa yake.

Kwa sasa hitmaker huyo wa ngoma ya “Mateke” hamfuati mume wake DJ MO kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo cha ndoa yao kuingiwa na ukungu ikiwa haijulikana.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke