You are currently viewing NE-YO AFUNGUKA SABABU YA ALBUM YAKE MPYA KUCHELEWA

NE-YO AFUNGUKA SABABU YA ALBUM YAKE MPYA KUCHELEWA

Mwanamuziki wa Marekani Ne-Yo ameelezea kilichochelewesha Album yake ya Nane “Self Explanatory” ambayo imetoka Ijumaa (Julai 15) Akizungumza kwenye mahojiano, Neyo alisema kwamba alichukua miaka minne kabla ya kuzindua Album nyingine kutokana na msongo wa mawazo uliotokana na janga la Corona.

Albamu yake ya saba kwa jina “Good Man” ilizinduliwa mwezi Juni mwaka 2018 na muda mrefu zaidi ambao amewahi kuchukua kutayarisha albamu baada ya kuzindua nyingine kabla ya hii ya nane ni miaka mitatu.

Ne-Yo alielezea kwamba maandalizi ya ‘Self Explanatory’ yalianza kabla ya janga la Corona na ikabidi yasimame kutokana na haja ya kuchagua kati ya muziki na kutetea maisha. Anasema muda wote wa janga la Corona muziki haukuwa akilini mwake na masharti ya kudhibiti janga yalipolegezwa alichukua muda kujirejesha katika hali ya awali kama mwanamuziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke