Wanamuziki nazizi na wyre wametangaza marejeo ya kundi lao la muziki Necessary Noize.
Nazizi kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza ujio wa EP yao mpya yenye nyimbo 8 za moto ambayo itaingia sokoni Mei 5 mwaka huu na kazi hiyo itapatikana pia kwenye majukwaa ya mitandaoni kama vile Spotify.
Nazizi amesema wamechukua muda mrefu kuachia EP hiyo kwa sababu walikuwa wameshikaka na majukumu mengine ya kibinafsi.
Kundi la muziki la Necessary Noize lilianzishwa mwaka 2000 na nazizi na wyre. Album yao ya kwanza ilitoka mwaka huo huo wa 2000, ilikuwa na nyimbo kama vile “Clang Clang” na “La Di Da.”
Album ya pili ya Necessary Noize iliyoitwa Necessary Noize II: Kenyan Gal, Kenyan Boy ilitoka mwaka 2004 na ilikuwa na nyimbo maarufu kama vile “Kenyan Gal, Kenyan Boy” na “Bless My Room.