Mwanamuziki nyota kutoka nchini Marekani Nelly ameomba radhi hadharani kufuatia kuvuja kwa video ambayo inamuonesha akiwa anafanya ngono ya mdomo (Oral Sex) na mwanamke mmoja.
Video hiyo ilipostiwa kwenye akaunti ya instagram ya Nelly Februari 8 mwaka huu na ilifutwa haraka lakini tayari ilikuwa imeshanaswa na kusambazwa mtandaoni.
Kupitia Instagram page yake Nelly ameandika kwa masikitiko “Ninaomba radhi kwa msichana huyu na familia yake, hiki ni kitendo ambacho hakikubaliki kwake hata kwenu pia. Hii ilikuwa ni video ya zamani ambayo ilikuwa ya faragha na haikukusudiwa kwenda kwenye hadhira.”