You are currently viewing NELLY THE GOOD AKIRI KUSHINDWA NA MUZIKI KISA MSONGO WA MAWAZO

NELLY THE GOOD AKIRI KUSHINDWA NA MUZIKI KISA MSONGO WA MAWAZO

Msanii wa Gengetone, Nelly the Goon amekiri hadharani kuwa anapitia wakati mgumu kwenye maisha kiasi cha kushindwa kuendelea na harakati za kuupambania muziki wake.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram msanii huyo ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba hali yake sio nzuri kwa sasa kwani ameathirika kiroho, kiakili na kiuchumi.

Mwanamuziki huyo wa Ochungulo Family amesema licha ya kuwa anasuasua kimaisha, amewataka mashabiki zake kutokataa tamaa kwenye muziki wake, hivyo waendelee kumweka kwa maombi ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

Hata hivyo hajaweka wazi ni kitu gani ambacho kinamsibu ila watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kumhurumia msanii huyo huku wakimliwaza na jumbe za kumtia moyo kutokana na changamoto zinazomuandama.

Utakumbuka Agosti 30 mwaka huu kundi la Ochungulo Family ambalo linaundwa na wasanii Nelly The Goon, Benzema na Dmore walitubariki na album iitwayo “Tamasha” ambayo ina jumla ya mikwaju 8 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke