You are currently viewing NEYO AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE KUVUNJIKA

NEYO AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE KUVUNJIKA

Mwanamuziki kutoka Marekani Ne-Yo ametoka hadharani na kuzungumzia Jambo ambalo jana mkewe Crystal Smith alilileta mtandaoni akisema ndoa yake na Mwanamuziki huyo imevunjika kutokana na vitendo vya usaliti.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ne-Yo ameomba faragha katika kulishughulikia jambo hili kwa maslahi ya watoto wake na familia yake kwa ujumla.

“Kwaajili ya watoto wetu na familia yangu kwa ujumla nitazitatua changamoto tunazozipitia kwa usiri. Mambo ya familia hayapaswi kuwekwa hadharani. Nawaomba muheshimu faragha ya familia yangu kwa sasa”

Crystal Smith juzi alishusha madai kwamba Ne-Yo amekuwa akifanya vitendo vya usaliti kwa kutoka na wanawake wanaojiuza tena bila kutumia kinga.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke