You are currently viewing NI RASMI SASA NADIA MUKAMI ANA UJA UZITO WA MPENZI WAKE ARROW BWOY

NI RASMI SASA NADIA MUKAMI ANA UJA UZITO WA MPENZI WAKE ARROW BWOY

Malkia wa muziki nchini Nadia Mukami pamoja na mpenzi wake Arrow Boy wanatarajiwa kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.

Wapenzi hao wawili wamethibitisha taarifa hiyo kwenye uzinduzi wa wakfu wao uitwao Lola na Safari ambao unalenga kuwasaidia akina mama wachanga kupata huduma nzuri ya afya ya uzazi.

Lakini pia wamedokeza kuwa walipata wazo la kuja na wakfu wa Lola na Safari kipindi ambacho Nadia Mukami alipoteza uja uzito wake mwaka wa 2021, hivyo wana mpango wa kuzindua kituo cha kuwahudumia akina mama wachanga ambao ukutana na changamoto wakati wa uja uzito.

Nadia Mukami amekuwa akikanusha madai ya kuwa na uja uzito licha ya mashabiki kusisitiza kuwa ana mimba ya Arrow Boy kutokana na kitendo chake cha kuvalia mavazi makubwa.

Utakumbuka Mapema mwaka huu hitmaker huyo wa ngoma ya maombi alifunguka kuwa alipoteza uja uzito wake mwaka wa 2021 lakini akahamua kutoweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake.

Mwezi agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu ambapo walienda mbali zaidi na kueleza kuwa waliahamua kuyaweka wazi mahusiano yao kwa sababu tayari walikuwa wamekuwa kiakili kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke