Ni Rasmi sasa mwanamuziki kutoka nchini marekani Rihanna ni mjamzito.
Mwimbaji huyo ambaye pia ni mwanamitindo anatarajia mtoto wake wa kwanza na rapa Asap Rocky.
Tovuti mbali mbali za nchini Marekani zimeripoti taarifa hii kufuatia picha ambazo zimewaonesha wawili hao wakiwa matembezini mjini New York wikendi iliyopita.
Mwaka 2019 ziliibuka taarifa kama hizi lakini alizikanusha kwenye mahojiano na Jarida la Vogue.
ASAP Rocky na Rihanna wamekuwa marafiki wa karibu katika kipindi cha muda mrefu kabla ya kuthibitisha hadharani kuwa wanapendana mwaka wa 2021.
Mwaka wa 2013, Rihanna alitokea katika video ya Asap Rocky ya “Fashion Killa” kama video vixen,jambo ambalo lilihusisha uwepo wa mahusiano ya kimapenzi kati yao.